TazamaRamaniTanzania

Lango kuu la utalii wa ndani katika mikoa nchini Tanzania

Kuwaelimisha na kuwahamasisha Watanzania wote kupenda mazingira, kuthamini urithi wa taifa, kutembelea na kutangaza vivutio vyetu vya asili na vya utamaduni, ili kuendeleza utalii wa ndani na kukuza fahari ya Tanzania.

Talii na Sisi

Gundua Mkoa Wako!

Je, unaufahamu mkoa wako? Chunguza vivutio vya utalii, tamaduni, historia na hazina za asili zinazopatikana katika kila mkoa wa Tanzania. Kila safari ni fursa ya kujifunza, kujivunia na kuitangaza nchi yetu.

Naipenda Tanzania, Najivunia Tanzania

Kila mkoa una historia yake, utamaduni wake na vivutio vya kipekee vinavyostahili kutembelewa.

Tazama Ramani Tanzania inalenga kuwaelimisha na kuwahamasisha Watanzania wote kupenda mazingira, kuthamini urithi wa Taifa na kutangaza vivutio vya utalii vya ndani kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Vivutio Vinavyoitangaza Tanzania Duniani

Kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro hadi tambarare za Serengeti na fukwe za Zanzibar, Tanzania imejaa vivutio vya kipekee vinavyovutia wageni kutoka duniani kote. Gundua maeneo haya na ujivunie urithi wa taifa letu.

Tazama Ramani Tanzaniainakualika kuchunguza vivutio maarufu vya nchi yetu vinavyoifanya Tanzania kuwa moja ya destinisheni bora za utalii duniani. Kila eneo lina historia, uzuri wa asili na uzoefu wa kipekee unaostahili kutembelewa.

Karibu Ndugu Mtanzania Mzalendo

"Usiulize Tanzania na Watanzania Watakufanyia nini. Jiulize Wewe Mwenyewe Binafsi Yako Kama Raia Halisia Wa Tanzania Na Mzalendo Halisia wa Taifa Tanzania

Utalifanyia Nini Taifa Na Watanzania Ili Siku Ambapo Utakapokufa na Kuiaga Tanzania Na Dunia,
Watanzania Wakumbuke Nyayo au Alama Na Urithi Wako na Kukulilia." - Thom GYPSY

 

Marais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Maswali na majibu ya ufahamu elimu, utali wa ndani kwa Umma wa Watanzania

Tunapokea maoni mbalimbali ya wadau wa utalii wa ndani na wanachi kwa ujumla wake katika kujenga na kukuza sekta hii ya utalii wa ndani.
Kama una ushauri wowote ule wa kujenga nchi yetu sote Tanzania kupitia utalii waweza kuwasilisha maoni hayo kupita barua pepe yetu; info@tazamaramaniutaliitanzania.co.tz | info@domestictourismsafaris.com | info@domestictourismsafaris.co.tz | edgardowelelo@yahoo.com

Je ni pamoja na Hifadhi za Taifa (National Parks), Mapori ya Akiba ya Wanyamapori (Game Reserves) , Hifadhi za Taifa za Misitu Asilia (National Natural Forests), Mabonde (Valleys), Milima (Mountains), Maeneo ya Kihistoria Tanzania (Tanzania Historical Sites), Makumbusho ya Taifa Tanzania (Tanzania National Museum), Bustani za Wanyamahai (Animal Zoos), Fukwe za Bahari (Beaches),Maziwa na Mito (Lakes & Rivers), Maporomoko ya Maji (Waterfalls), Miji ya Kihistoria (Historical Towns), Matamasha mbalimbali (Festivals) , Maonyesho (Trade Fairs) ,Riadha (Marathon), Ngoma za Asili (Traditional Dances), na maeneo yenye historia za zama za mawe (Archaeological Sites) au kwingineko?

Kunapatikana faida nyingi kwa raia wa Tanzania katika kuvitembelea na kujionea vivutio vya utalii;

i) kujifunza mambo mbalimbali

– kunapatikana mambo mbalimbali ya kujifunza kama mtalii wa ndani hususani kwa wanachuo, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, pia pamoja na wananchi kwa ujumla wake.

ii) Kupumzisha mwili na akili

– majukumu ya kila siku ya mwanadamu yamekuwa mengi kiasi cha kufanya watu kushindwa kupata muda wa kupumzika, na mara nyingine kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya digitali watu wamekuwa wakitumia muda wa kupumzika katika matumizi ya simu ambayo pia yanachosha akili. Njia nzuri na bora ya kupumzisha mwili na akili ni pamoja na kutoka katika eneo lililozoeleka kwenye ratiba ya kila siku. Iwapo utapanga muda mara moja wa wiki au mara moja kwa mwezi kutembelea mojawapo ya vivutio vya utalii utaweza kurudi ukiwa na akili iliyo mpya na kuongeza ufanisi kwenye majukumu ya kila siku. Wengi wamejaribu mbinu hii na kuweza kufanikiwa sana.

iii) kujionea maajabu mbalimbali na vitu vipya

– Utalii una mabo mengi mapya na mazuri ambayo binadamu anaweza kujifunza na kufurahia.

iv) Kujaribu vitu ambavyo haujawahi kuvifanya maishani

kama kujaribu kuogelea kwenye maziwa na mito. Kujaribu kucheza ngoma za kabila tofauti na la kwako. Kujaribu kufanya matembezi ya miguu ndani ya mapori ya akiba ya wanyamapori, misituni au hifadhi za taifa (National parks).

v) Kujenga afya ya mwili na akili

hususani ukiwa umetembelea maeneo yanayokutaka kutembea kwa miguu mfano ndani ya hifadhi za taifa (National parks), au katika mapori ya akiba ya wanyamapori (Game reserves).

Vi) Kufurahia na kuburudika uumbaji wa Mwenyezi Mungu

– Mwenyezi Mungu ameumba dunia na vitu vyote vilivyoujaza ulimwengu kwa jinsi ya ajabu nay a kushangaza sana. Unapoenda kutalii unapata nafasi ya kuufurahia uumbaji wa Mungu kama vile Maporormoko ya Maji, Mabonde , Mito mikubwa na midogo, Misitu ya asili iliyo ya aina mbalimbali, pamoja na milima.

Kwa kuwa utalii ni sekta mtambuka: pindi Mtanzania anapotembelea na kujionea vivutio vya utalii kwa njia moja ama nyingine atahusika moja kwa moja na mambo ya usafiri, chakula, malazi, pamoja na ununuzi wa bidhaa mbalimbali hivyo kuwezesha kuongezeka kwa pato la Taifa letu Tanzania, kipato cha mtu mmoja mmoja, ajira kwenye sekta za huduma za utalii pamoja na kusaidia uelewa na ufahamu wa vivutio vya utalii kwa wananchi hivyo kuongeza hali ya uzalendo kwa Watanzania.

Ni pamoja na Hifadhi za Taifa (National parks):
Tanzania ina jumla ya Hifadhi za Taifa 21 kwa upande wa Tanzania bara na 1 iliyo pekee visiwani Zanzibar inayofahamika kama β€˜β€™Jozani Chwaka Bay National Park’. Hifadhi za Taifa kwa upande wa Tanzania bara ni pamoja na Arusha, Tarangire, Ziwa Manyara, Saadani, Mkomazi, Mikumi, Ruaha, Kitulo, Katavi, Udzungwa, Burigi – Chato, Saanane, Nyerere, Gombe, Kisiwa cha Rubondo, Mahale, Ibanda – Kyerwa, Rumanyika – Karagwe, Serengeti,Ugalla,pamoja na Mlima Kilimanjaro.

Hata hivyo, kusini mwa Tanzania unaweza kutembelea Hifadhi za Taifa ambapo katika kila Hifadhi utakutana na upekee wa aina yake kama vile Maporomoko ya Maji ya Sanje katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa mkoani Iringa na Morogoro, wanyamapori swala aina ya kudu wakubwa na kudu wadogo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa. Ndege wazuri wenye kupendeza na kuvutia na pia maua maarufu kama vile bustani ya Mungu katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, pamoja na Mabwawa na Mito mizuri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na bila kusahau makundi makubwa ya wanyamapori Nyati au Mbogo katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro. Viboko, Mamba na Mto mkubwa wa Rufiji ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere mkoani Pwani, Morogoro, pamoja na Lindi.

×